Kiungo wa Ivory Coast Yaya Toure anakaribia kupata mkataba mpya katika klabu yake ya Manchester City baada ya kocha wa timu hiyo Guardiola kuonyesha kuhitaji huduma yake.
Toure alionekana kama hana umuhimu tena klabuni hapo baada ya kuachwa nje katika kikosi kilichocheza michuano ya Ulaya na hakucheza michuano ya ligi ya England mpaka mwezi Novemba.
Lakini kadri siku zilivyokwenda alianza kuwa na umuhimu klabuni hapo na baadaye kurejea tena kuwa muhimuli wa timu hiyo.
Wakati huo huo Guardiola amemtaja mlinzi wake wa kulia Pablo Zabaleta kama shujaa kamili wa klabu hiyo baada ya Muargentina huyo kutangaza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
City wataufanya mchezo wa mwisho dhidi ya West Brom kuwa wa kipekee kwa Zabaleta kabla ya kutoa mkono wa kwaheri.
No comments:
Post a Comment