Breaking

Tuesday, May 16, 2017

PROF JOOYCE NDALICHAKO ASIMAMISHA WATENDAJI WAWILI

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako amewasimamisha kazi Kaimu Kamishna wa Elimu, Nicholas Bureta na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Tanzania, Dr. Elia Kidga kufuatia sakata la kasoro zilizopo katika vitabu vya kujifunzia wanafunzi.

Prof. Ndalichako ametangaza kuwasimamisha kazi watu hao kufuatia mjadala uliobika bungeni kuhusu kasoro kwenye vitabu hivyo ambavyo vimechapishwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kufundishia.
“Kwa mamlaka niliyonayo, ninamuagiza Kaimu Kamishna wa Elimu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, kuondoka ofisini mara moja ili kupisha uchunguzi,” alisema Ndalichako
Waziri Ndalichako amewasimamisha viongozi hao na ameliambia bunge kuwa uchunguzi wa kina unafanyika na baada ya kukamilika hatua za kinidhamu na kisheria zitachukuliwa dhidi ya wote waliohusika.
Na Emmy Mwaipopo


No comments:

Post a Comment