Breaking

Tuesday, May 16, 2017

FAHAMU FAIDA ZA KITUNGUU SAUMU KWENYE MWILI WAKO

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaaluma, huitwa allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umeng’enyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuepua mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake.
Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
Kigawanyishe katika punje punje 6
Menya punje moja baada ya nyingine
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa.
Haya ni baadhi ya magonjwa yaliyothibitika kutibika na yanatibika au kukingika na kitunguu swaumu:
Huondoa sumu mwilini, Husafisha tumbo, Huyeyusha mafuta mwilini (Cholestrol), Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I, Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine, Huzuia kuhara damu (Dysentry), Huondoa Gesi tumboni, Hutibu msokoto wa tumbo, Hutibu Typhoid, Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi, Hutibu mafua na malaria, Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu, Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume), Hutibu maumivu ya kichwa, Hutibu kizunguzungu, Hutibu shinikizo la juu la damu, Huzuia saratani/kansa, Hutibu maumivu ya jongo/gout, Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, Huongeza hamu ya kula, Huzuia damu kuganda, Husaidia kutibu kisukari, Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
Sifa kuu za kitunguu swaumu ni kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni pamoja kuwa na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
a. Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
b. Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
c. Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
d. Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.
KUMBUKA :
Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie vitunguu swaumu kwani vinaweza kusababisha madhara.
Chanzo Dr. Fadhili Paulo



5 comments: