Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry amesema kuwa huenda akastaafu baada ya kuwasaidia mabingwa hao wapya wa EPL kuilaza Watford kwa magoli 4-3 katika dimba la Stanford Bridge.
Terry ambae kwa sasa ana umri wa miaka 36 amefunga goli la kwanza katika mchezo, anatarajia kuondoka mwishoni mwa msimu huu.
Mabingwa hao watakuwa wenyeji wa klabu ya Sunderland siku ya Jumapili, ikiwa ni mchezo wao wa mwisho kabisa kwa msimu huu.
Terry ameichezea Chelsea michezo 716 tokea mwaka 1998.
Ameisaidia Chelsea kushinda vikombe vitano vya FA, Vitatu vya Ligi ya EPL, kombe la mabingwa Ulaya mara moja na Europa ligi mara 1. Hivyo kwake hakuna alichobakiza katika tansia nzima ya soka.
No comments:
Post a Comment